1. Ningewapumbaza sana waone rangi yao nyeusi ni mbaya, hii ingewafanya wajiradharau na kumheshimu yeyote mwenye rangi isiyo nyeusi. Ningewafanya waheshimu kila mzungu hata kama hana tabia nzuri. Ningepumbaza akili za viongozi wao wawapende na kuwakaribisha wazungu mpaka maofisini mwao bila kuwasumbua.
2. Ningewafanya waongo na waliojaa majungu, ningewachochea kwenye akili zao wapende kuzungumzia maisha ya watu na kusahau habari za maendeleo. Ningewafanya wakubwa kwa wadogo kutumia muda wao mwingi kuzungumzia mahusiaono ya watu na hasa yale yahusuyo ngono. Ningewafanya wanaume wawe wajinga na wajisifu kwa ngono. Na wanawake ningewafanya wavae nusu uchi ama nguo za kubana nabado wajione wana akili timamu na wakisasa zaidi. Ningewafanya wanawake waliosoma watetee uvaaji huu kwa udi na uvumba kwa visingizio vya haki za binadamu. Ningewafanya wamwone mtu asiye shabikia masuala ya ngono mshamba na asiye kwenda na wakati. Ili kupata wafuasi wengi, ningelifanya swala la ngono lizungumzike hata mbele ya watoto wadogo na karibu kila mtu atabasamu kama hakusema lolote. Vilevile kutimiza lengo la kupata wafuasi wengi ningewafanya wanandoa kuona si tatizo sana kutoka nje ya ndoa. Ningewafanya vijana waone ni kawaida sana kuwa na mahusiano ya ngono kabla ya ndoa, na hata wasijiite malaya bali wajanja.
3. Ningewafanya wajinga kiasi cha kujidanganya wenyewe, kukazia maarifa ningewafanya viongozi wao watetee ujinga ili mradi ujinga ule umesemwa ama kufanywa na mtu wa kambi moja ama rafiki.
4. Ningewaficha akili ya kuwaza kujitegemea, ningewafanya wafikiri kusaidiwa na mataifa mengine, katika hili ningeanza na mtu mmoja mmoja, familia, taasisi mpaka Taifa husika.
5. Ningewafanya waliosoma na wenye fedha wajione ni wamaana sana kuliko wasiosoma na maskini. Hili lingewaondolea umoja, lakini pia lingeongeza chuki kati yao.
6. Ningewafanya waoneane wivu wa kijinga, ningewafanya wasipende wenzao wawafikie katika elimu ama utajiri walioufikia. Hili lingewarudisha nyuma sana kimaendeleo.
7. Ningewafanya wanafiki sana, ningeifanya akili yao iwaze kuwaheshimu watu wenye vyeo ama matajiri. Ningewafanya wajinga kiasi cha kutokumsalimu maskini ama mtu wa cheo cha chini. Ningewafanya juha hata kuwakana wazazi wao waliovijijini sababu ya kuchoka kwao.
8. Ningewafanya wajinga kiasi cha kuvaa vitu vya thamani ili wenzao wawaone wana uwezo kifedha hata kama siyo kweli.
9. Ningewafanya wengi waende makanisani na misikitini kama fashion tu lakini wafanye mambo ya ajabu kwenye maisha yao ya kawaida.
10. Ningewafanya wajinga kiasi cha kudharau kila kitu cha kwao, ningewafanya wasizipende lugha za kwao, na utamaduni wao. Ningeifanya kila familia iwe na TV yake ili waweze kuiga vizuri mambo ya wazungu. Ningewafanya watoto na vijana wapende sana tamthiliya za kizungu ili kufuta kabisa uafrika kwenye bongo zao.
umeongea ya kweli hapo manake wako wengi wanamna hiyo,mbona umesahau wakusema wanunue vitu vya kifahari wakiwa nje ya nchi wakati ndugu zao afrika wanakufa njaa,na hata senti ya kununua vidonge vya maralia akuna.
ReplyDelete